THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGIES COMMISSION

Uzinduzi wa Kongamano la Saba la Tehama 2023

  • News

Tume ya TEHAMA imezindua rasmi kongamano la saba la TEHAMA litakalofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 mpaka 20 Oktoba 2023. Kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Unleash emerging technologies in the digital transformation for job creation and socio-economical development". Kauli mbiu hiyo itagusa teknolojia mbalimbali zinazotambulika kama emerging technology "teknolojia chipukizi". Miongoni mwa teknolojia hizo ni pamoja na Artificial Intelligence "akili bandia" kwa ajili ya kutengeneza kazi kwa vijana na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kongamano hilo la saba ni kiungo kikubwa kinachowaunganisha waekezaji, wabunifu, wataalam, waajiri, vijana, nakadharika. Katika mkutano huo na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amezindua pia Kadi maalum kwa ajili a wataalam wa TEHAMA na washiriki wa kongamano ya mwaka la TEHAMA. Kadi hiyo yenye microchip inauwezo wa kumtambulisha mtaalam aliyesajiriwa na TUME ya TEHAMA na pia washiriki wote wa kongamano hilo wa ndani na nje  ya nchi. Kadi hizo zinamatumizi mengi ya kijamii pia. Kwa mara ya kwanza zitatumika kwenye Kongamano la saba.