THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGIES COMMISSION

Taarifa kwa Kampuni za Bunifu za TEHAMA

  • News

TUME YA TEHAMA inapenda kumpongeza Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa kibali cha kuruhusu wafanyabiashara wanaoanzisha biashara mpya ikiwemo kampuni za bunifu za TEHMA kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Taarifa ya mabadiliko haya ilitolewa rasmi tarehe 8 Machi 2023 na Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Dodoma katika Wilaya ya Kondoa.


Tafiti zinaonyesha kuwa karibu asilimia sabini 70% ya biashara mpya hushindwa kuendelea ndani ya miaka mitatu ya kwanza. Hivyo kwa hatua hii tunategemea kuona biashara changa zikishamiri kwani kutaongeza mitaji ya kuzungusha kwenye biashara na kampuni hizo na hivyo kuongeza ajira kwa vijana na wanawake wengi nchini.
TUME YA TEHAMA tunatambua jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita za kuhakikisha inakuza kampuni za bunifu za TEHAMA nchini chini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kampuni changa na uwekezaji nchini MKUMBI (Blueprint). Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika utekelezaji wa MKUMBI ikiwemo ufutaji na upunguzaji wa tozo, faini na ada, upitiaji na urekebishaji wa Sheria; uunganishaji na uondoaji wa urudufu wa majukumu miongoni mwa mamlaka za udhibiti nk.