THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGIES COMMISSION

Hafla ya Utiaji saini Mkataba wa Ushirikiano katika sekta ya Tehama kati ya Tume ya TEHAMA Tanzania na Kampuni ya Aron Group Tanzania

  • News

Tume ya TEHAMA Tanzania (ICTC)  imesaini Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Tehama nchini na Kampuni ya Aron Group Tanzania Limited mnamo tarehe 05 April, 2023,

Akifungua hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema katika Kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakua na Kuongeza pato la Taifa hatuna budi kuziunga mkono Taasisi changa za TEHAMA zinazochipukia (Startups) ili ziweze kuwa chachu ya ajira kwa vijana na kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali nchini.

"Sisi kama Tume tutaendelea kuhakikisha upatikanaji wa Huduma za kidijitali katika mifumo ya miamala ya pesa inakua ya uhakika na yenye kikudhi usalama wa pesa za mtumiaji" Alisema Dkt. Nkundwe.

Aidha Dkt. Nkundwe ametoa wito kwa makampuni mengine kuja kwa wingi kuwekeza nchini hasa katika sekta hii ya TEHAMA kwani wameandaa Mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Kwa upande wa Aron Group Tanzania Limited Bw. Leonce Mongi amesisitiza kuwa kuanzishwa kwa mfumo huu wa malipo wa Shake App utakua msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kwani wataweza kukusanya taarifa za mapato na matumizi kupitia mfumo huu na hivyo kuwa na historia nzuri ya miamala wafanyayo.

Vilevile kupitia Mfumo huu wa Shake App mfanyabiashara ataweza kutangaza biashara zake na kuwavutia wateja mbalimbali na hivyo kuongeza mauzo zaidi alisema Mongi 

"Niwahakikishie watumiaji wote mfumo huu ni salama na rahisi kwa mtumiaji, mfumo huu umekidhi vigezo na masharti yote ndio maana leo hii tumekuja kuutambulisha hapa Tume ya Tehama Tanzania." - Mongi

Mwisho.