THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGIES COMMISSION

TUME YA TEHAMA YAZINDUA WIKI YA JUKWAA LA 5 LA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA (5TH INNOVATION AND TECH FORUM)

  • News

Nukuu za Naibu waziri wa WIZARA YA HABARI MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI. DR KUNDO ANDREA MATHEW katika uzinduzi huo zilikuwa kama ifuatavyo: " Tanzania tuna mpango wa kuwa na satellite yetu lakini tutafikaje huko, basi ni kupitia ubunifu na technolojia" Tupo kwenye kipindi cha teknolojia swala ni namna gani tunaweza kukopi na kwenda na mabadiliko haya ya teknolojia. Najua Wote tupo hapa kwa ajili ya mjadala na naamini tunajua kabisa ili tuendelee kwenye nyanja ya teknolojia tunahitaji Ubunifu na sera ambazo zinatekelezeka kuukuza ubunifu huo. Najua Wote tupo hapa kwa ajili ya mjadala na naamini tunajua kabisa ili tuendelee kwenye nyanja ya teknolojia tunahitaji Ubunifu na sera ambazo zinatekelezeka kuukuza ubunifu huo. Tunachotazamia hapa sio sera tu bali na namna bora ya kuendana na hizo sera na sisi tutayabeba tuone namna bora ya kwenda kuyatekeleza. Leo la serikali ni kuangalia namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na jamii katika nyanja za technolojia. Lengo la Serikali ni kuangalia namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na jamii katika nyanja za teknolojia.

Nukuu za Mkurugenzi Mkuu wa TUME YA TEHAMA DKT.NKUNDWE MOSES MWASAGA.

Ni heshima kubwa kwangu kuwepo mbele yenu siku ya leo kuzungumza nanyi katika Jukwaa hili la Ubunifu na Teknolojia. "Uchumi wa kidigitali unaendana na ubunifu katika sekta ya TEHAMA lakini pia ili kuwepo na ubunifu wenye tija kwenye uchumi wa kidigitali basi tunahitaji kuwepo na sera nzuri na rafiki zinazotekelezeka". "Kufanya ubunifu wa Software Applications (Mfumo) ni jambo moja lakini kuwepo na data sahihi ndio jambo muhimu zaidi ili kuufanya ubunifu huo ufanye kazi".