Tume ya Tehama kuendeleza wabunifu nchini
Arusha, Serikali kupitia Tume ya Tehama imeanza kutekeleza mpango wa kukuza na kuendeleza wabunifu wa Tehama nchini kwa kuanzisha vituo kila mkoa ili kuwawezesha vijana kupata sehemu maalumu ya kuweza kuendeleza bunifu zao kwa njia ya Tehama.
Hayo yamesemwa leo Februari 28, 2023 jijini Arusha Katibu Tawala msaidizi uchumi na mzalishaji Mali mkoa wa Arusha, Daniel Loiruck wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa ubunifu katika Tehama uliowashirikisha vijana zaidi ya 150 kutoka mkoani Arusha.
Amesema kuwa, mkutano huo unalenga kujadili mashauriano na kubadilishana uzoefu katika kuanzisha na kuendesha shughuli za ubunifu kwa kutumia TEHAMA.
Source: Happy Lazaro